Maswali na Majibu.

Uliza Maswali inshALLAH kwa uwezo wa ALLAH SWA utajibiwa haraka iwezikanavyo na Sheikh Jabir Yusuf Katura au Sheikh Hamza Mansoor wa Masjid Ijumaa Mwanza  Tanzania.

By Ahmed Ahlusuna TV Mwanza Tanzania.

36 responses to “Maswali na Majibu.

  1. Manshallah ni program nzuri sana mie kwa sasa sina la kuuliza lakini nimefurahi sana kupata tovuti kama hii ya kiislamu ManshaALLAH ALLAH awalipe kila lakheyri ameen.

  2. Assalaamu ‘alaykum

    Naomba niulize hivi: kuweka jino la bandia ni halali? mfano sehemu una pengo sasa unataka kuweka jino la bandia

    wahadha salaamu ‘alaykum

    Salum

  3. Bwanakombo Nabahany

    Alhamdulillah, sifa zote niza Allah (Swt) namshukuru tena Allah (Swt) kwakunijaaia kubahatika kupa tovuti ya Ahlusuna. Natowa shukurani zangu za dhati kwa kunipokea kama mwanafunzi wenu na Inshallah nitafaidika kupitia kwenu. Allah awalipe kila la kheri na iwe ni miongoni mwa ahsanati zenu siku ya kiyama (malipo) Inshallah. Shukran. Fy amani llah salama.

  4. je kuna fatwaa gani kwa musalmu asie sali ? i mean …ana haki ya kuambiawa si muislamu au atakua ni muislamu jina tu ?

  5. khamisi abdi othmani

    a,w,w.furaha iliyoje moyoni mwangu,namshukuru allah s.w.t. Kwakukupeni tawfiq ya kuanzisha tovuti hii.mimi ni mwanaharakati wa da’awa vijijini nikiwa imamu na ust masjid umar bn khatwabi kijiji cha nyakabindi wilaya ya baliadi kwa miaka 6 sasa.aliyenipeleka huko ni sheikh jabily katura,ombi langu kwenu wanadaawa wenzangu nakabiliwa na changamoto2.1- tunaujenzi wa msikiti natumefikia hatua ya msingi na kujenga msingi lakini nguvu zetu ni ndogo. 2- ugumu wa maisha unaonikabili kutokana na posho kutokidhi kwani napanga naninalazimika kulipia umeme.mkiwa ahlu sunna watawhid naomba msaada kwa allah kisha kwenu. Wallahu waliyu tawfiq.

  6. Aww. Shukran kwa tovuti hii ya ki islam Allah akulipe kila la kheri. Amin. Swali: vipi ku husu jamaat tabligh? Mfumo wanao utumia una ushahidi?

  7. Salaams

    napenda kujua kama mtume aliona mke wa miaka sita na kuanzakumuingilia akiwa na miaka 9

    abunaser

  8. Assalam alaykum ningependa kufahamu maji ya pepo za alla na daraja zake

  9. Asalam alaykum,ninaomba ALLAH awawezeshe kwa juhudi mlioifanya.

  10. Assalaam alaykum Allah awajaalie kuanzisha jambo ambalo watu wengi wanalitumia kwa sasa hasa waofisini nadhani itawarahisishia kwani kwao ni nadra kuhudhuria misikitini na kwenye makongamano mbalimbali ya dini.

  11. Asalam aleikum warahmatullahi wabarakatu sheikh swali langu ni nataka kujua kwa nini ninaposoma quran hutokwa machozi au kusikizanikitega mashkio nisijishughulishe pia machozi hunitoka naomba jawabu tafadhali

  12. zipi sifa za imamu?

  13. asalaam alehkhum,mimi swali langu ni kwamba, mfano umefikia kipindi cha kuoa na huyo bint unatetaka kumuoa uliisha wahi kuzini nae.swali langu ni kwamba je,ikiwa ninahitaji kumuoa huyu binti ni nini hukumu yake ktk qur’an na hadith za mtume ili zikitekelezwa hizo tu huyu bint unakuwa unauwezo wa kumuoa?

  14. Qur-an ameshushwa yote katika mwezi wa ramadhan?

  15. Assalam Aleykum,ni Jambo Gani Nifanye Ili Aliyetangulia Mbele Ya Haki Afaidike?

  16. Assalaam alaikum. Vipi hali zenu? Naombeni munisaidie majibu ya maswali yangu….. nahitaj kufaham swahaba gani alikufa bila kuoa? Na neno pepo limetajwa mara ngapi? Inshallah naomba munisaidie. Wabillah tauwifiq

  17. layla abdulaziz

    Salaam alayk, naomba niulize swali dada angu anamwaka wa pili nyumban hajapewa talaka na mumewe hamtaki kwake na hataki kutoa talaka. Nisaidie nimshaur dada yangu nini hukmu yake kisheria anafaa kuolewa tena rizki zipo nyingi ila jibu hatujui la kujibu

    • Waleykum salam Warahmatullahi Wabarakatu.

      KUTAKA TALAKA BILA YA KUWEPO TATIZO NI JAMBO LILILOHARAMISHWA KISHARI’AH:

      Mara nyingi mwanamke anataka talaka kwa mume wake pindi wanandoa wawili wanapomwachia Shaytwaan nafasi na pindi ghadhabu ya mwanamke inaposhtadi, lau angesubiri kidogo na kuzuia ghadhabu zake na kupata utulivu angeona kuwa hakukuwa na sababu ya hilo, talaka si jambo la mzaha wakalichezea wanandoa, akawa mmoja wao akighadhibika anamtishia mwenzake kwa talaka na mwengine akisema anapoghadhibika, ‘Nitaliki’.

      Wanandoa wanatakiwa kuwa ni werevu kuliko matatizo yanayowakabili, wakishirikiana katika kutatua matatizo na wakifahamiana vizuri kwa hilo, na kila mmoja anajaribu kushusha mahitaji yake na kuachana na misimamo yake ili jahazi lisije likazama. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam.) amemtahadharisha mke asidai talaka kama hamna tatizo la msingi kwa kusema,

      “Mwanamke yeyote atakaye talaka kutoka kwa mume wake bila ya tatizo la msingi basi ni haramu kwake kunusa harufu ya pepo”[Hadith: Imepokewa na Ahmad na At-Tirmidhiy na wengineo]

      Hata hivyo kungekuwa na jambo lingine linalopelekea jambo hili kwa mfano mume kuwa na tabia mbaya kiasi cha kuwa mke wake hawezi kuvumilia, au ni mtu fasiki asiyetekeleza haki za mke wake na watoto wake, au mfano wa hayo katika mambo yanayofahamika kisheria na desturi.

      Mke anaweza kudai talaka ikiwa njia zote za kufanya suluhu baina yao ndani ya nyumba na hata nje zimeshindikana ambazo katika utatuzi wenyewe na suluhu yenyewe hushiriki hakimu kutoka upande wa mume na hakimu kutoka upande wa mke kushindikana.

      Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema,

      “Na mkichelea kuwepo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu Atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari.” (4:35)

  18. nini ubaya wa dhehebu la kishia?

    • IMAAM ASH-SHAAFI’IY

      Imam Shafi’iy alisema siku moja kuhusu Mashia, ‘Sijawahi kuona miongoni mwa makafiri watu wanaojulikana kwa kusema uongo kuliko Mashia.’ [Minhaaj as-Sunnah an-Nabawiyyah, 1/39] Wakati mwingine alisema, ‘Simulia elimu kutoka kwa yeyote yule utakayekutana naye isipokuwa Mashia, kwani wao hutunga Hadyith na kuzifanya sehemu ya Dini yao.’ [Minhaaj as-Sunnah an-Nabawiyyah, 1/38].
      IMAAM ABU HANIYFAH

      Imesimuliwa kuwa Imaam Abu Haniyfah alikuwa akikariri kauli ifuatayo kuhusu Mashia, ‘Yeyote mwenye mashaka kuhusu ukafiri wao basi nae pia ni kafiri.’
      IMAAM MAALIK

      Siku moja Imaam Maalik aliulizwa kuhusu wao (Mashia) akajibu, ‘Usiongee nao wala kupokea hadithi zao, kwani hapana shaka wao ni waongo.’ [Minhaaj as-Sunnah, 1/37] Ilitajwa katika darsa yake kuwa Mashia wanawatukana Maswahaba. Katika kujibu akataja ayah: ‘‘Muhammad ni Mtumwa wa Allaah na waliokuwa naye ni wakali dhidi ya makafiri na wenye kurehemeana wenyewe kwa wenyewe. Ili kuwachukiza makafiri…’’ Kisha akasema, ‘Basi yeyote anayebughudhiwa wakati Maswahaba wanapotajwa basi na yeye kakusudiwa pia na ayah hii.’ (Yaani yeyote anayechukizwa kwa kutajwa Maswahaba basi amekusudiwa katika Aayah hii kwa sababu Allaah Anasema, ‘‘Ili kuwachukiza makafiri…

  19. A./alaykum!
    Hapa kuna ‘Shubha’ naomba ufafanuzi kuhusu aya ya qur an iliyopo ktk
    Al Nahl namba 43 na ktk Anbiyaa namba 7, inasema
    …BASI WAULIZENI WENYE KUMBUKUMBU IKIWA NYINYI HAMJUI.
    Je ninani hao wenye kumbukumbu waliokusudiwa hapa?
    Mashia wanadai aya hii ilishuka kuwatambulisha Ahlul Bait nao ni Ali, Fatma, Hassan na Hussein!

  20. Assalam alykum
    Ni swahaba yupi wa MTUME S.A.W alikataa kuuguzwa na mshirikina?
    Ni msikiti upi wa kwanza kusomwa QURAN?
    Ni swahaba yupi alikufa akiwa anatawadha?
    Neno pepo limetajwa mara ngapi ndani ya QURANI?
    Neno ANNAR limetajwa mara ngapi ndani ya QURANI?

  21. Nitamtibuje mtu aliyechanganyikiwa na mashetani?

  22. Nina maswali matatu :- 1.ni swahaba yupi aliekataa kutibiwa na mshirikina ? Swali 2 .ni msikiti upi wakwanza kusomwa Quraan ? Swali 3.ni swahaba yupi aliekufa anatawadha ?.

  23. Maashallah ni program nzuri sana natamani nipate tovuti

  24. Whch sahaba died whle not maried

  25. addy mohammed shariff

    Neno pepo limetajwa mara ngapi katika Quran

  26. Assalamu alayku warahma tu llahu wa barakatu, ndugu zangu waislamu naomba muni saidie katika matatizo haya nilio nayo, niko na suali, mume wangu aliwachana na mke wake kisha aka ni owa Mimi baada ya miaka kumi na Tano waka rudiana na Mimi nili ishi nacyeye katika shida na mpaka sasa tuko na matatizo ya kimaisha lakini Mimi na simama na yeye bega kwa bega na Yule mke mwenzangu yeye kwao ni tajiri lakini hataki kusaidiana na mumewe hata watoto wake Mimi ndie naishi nao sasa mume wetu akipata kitu chochote ni lazima agawe sawa kwa sawa ?

  27. Nabii gani aliekataa kuuguzwa na mshikina (2) swahaba gani aliefariki bila kuowa (3) fimbo ya nabii mussa ilikuwa ni ya mti gani

Leave a reply to ahlusuna Cancel reply