Ukhalifa Wa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘Anhu)

Mara baada ya kutangazwa kufariki kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Abu Bakr alikwenda moja kwa moja mpaka mahali alipolazwa, akaufunua uso wake na kumbusu juu ya kipaji cha uso wake baina ya macho yake, kisha akasema;

“(Nakufidia) Kwa baba yangu na mama yangu, unapendeza ukiwa hai au umekufa”.

Kisha akaufunika uso wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), akanyanyuka na kupanda juu ya membari na kusema;

“Kama yupo aliyekuwa akimuabudu Muhammad, basi Muhammad kesha kufa, ama kama mlikuwa mkimuabudu Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu yuhai na hafi. (kisha akaisoma kauli ya Mwenyezi Mungu ifuatayo;)

“Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume tu. Wamepita kabla yake Mitume (wengi kabisa). Akifa au akiuawa ndiyo mtarudi nyuma (kwa visigino vyenu), muwe makafiri kama zamani? Na atakayerudi nyuma kwa visigino vyake hatamdhuru Mwenyezi Mungu cho chote. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaomshukuru”.

Aali ‘Imraan – 144

Watu wakawa wanalia na wengine wakawa wanatembea mitaani huku wakiikariri aya hiyo. Anasema Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu);

“Ilikuwa kama kwamba hatujapata kuisikia aya hiyo isipokuwa wakati ule (kama kwamba tunaisikia kwa mara ya mwanzo)”.

Al-Bukhaariy – kitabu cha Fadhila za Maswahaba.

Juu ya kuwa Qur-aan ilikwisha kamilika kabla ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kabla ya kufariki kwake, lakini aya hii ilikuwa kama ni mpya kwao, kamakwamba hawakupata kuisikia kabla ya siku hiyo kutokana na mshituko waloupata kwa kifo cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Al-’Abbaas bin Abdul Muttalib na ‘Aliy bin Abi Twaalib na Az-Zubayr bin Al-‘Awaam (Radhiya Allaahu ‘anhu) ndio waliofanya kazi ya kumuosha na kumkafini Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kumshughulikia mpaka aliposaliwa, na hii ni kwa sababu Al-’Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni ‘Ami yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni mtoto wa ammi yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na Az-Zubayr (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni mtoto wa shangazi lake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kwa ajili hiyo wao ndio waliostahiki zaidi kujishughulisha na hayo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s