Aqiydah Swahiyh Ya Muislamu

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Swahiyh Ya Muislamu

SWALI

JIBU

DALILI KUTOKA QUR-AAN

DALILI KUTOKA HADIYTH

1- Kwa nini Allaah Katuumba? Katuumba Ili tumuabudu na tusimshirikishe Naye kwa chochote.

 (وماخلقت الجن والإنس إلا ليعبدون)   

Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.(Adh-Dhaariyaat: 56)

 حق الله على العباد أن يعبدوه ولا يشركوا به شيئا (

Haki ya Allaah kutoka kwa mja wake  (mja anapaswa kumfanyia) ni kumuabudu bila ya kumshirikisha..

2- Jinsi gani tumuabudu Allaah سبحانه وتعالى Kama Alivyotuamrisha Allaah na Mtume صلى الله عليه وسلم  kwa ikhlaas

 (وما امروا إلا ليعبدوا الله مخلصين له الدين)  

Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Allaah kwa kumtakasia Dini. (Al-Bayyinah: 5)

 (من عمل عملا ليس عليه أمرنا

 فهو رد )

Atakayefanya kitendo kisichokuwa chetu (kisicho katika  Dini) kitarudishwa (hakitakubaliwa).

3- Je, tumuabudu Allaah سبحانه وتعالى kwa kumuogopa (adhabu Yake) na kutumaini (pepo Yake)? Ndio tunamuabudu kwa kumukhofu na kuwa na matumaini

(وأدعوه خوفا وطمعا  (أي خوفا من ناره وطمعا في جنته   

Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai (kukhofu moto Wake na kutumaini pepo Yake).(A’araf: 56)

 (اسأل الله الجنة وأعوذ به من النار)

Namuomba Allaah Pepo na najikinga Kwake na moto.

4- Nini Ihsaan katika ibada? Kujichunga (kuwa makini) katika ibada kwa ajili Yake Allaah سبحانه وتعالى Pekee.

  (ان الله كان عليكم رقيبا)  النساء

 (الذي يراك حين تقوم) الشعراء

Hakika Allaah ni Mwenye kuwaangalieni. (An-Nisaa: 1)

Ambaye Anakuona unaposimama. (Ash-Shu’araa: 218) 

(الإحسان أن تعبد الله كانك تراه فأن لم تكن تراه فأنه يراك )

Ihsaan ni kumuabudu Allaah سبحانه وتعالى kama vile unamuona, na kamahumuoni basi Yeye Anakuona.

5- Kwa nini Allaah سبحانه وتعالى Ametuma Wajumbe (Mitume)? Kutuita katika kumuabudu na kuepukana na kumshirikisha.

 (ولقد بعثنا في كل أمة رسولا أن اعبدوا الله وأجتنبوا الطاغوت)

Na kwa hakika kwa kila ummah tuliutumia Mtume kwamba, Muabuduni Allaah, na muepukeni shaytwaan. (An-Nahl: 36)

والانبياء إخوة ودينهم واحد(

Na Manabii ni ndugu na dini yao ni moja.

6- Nini Tawhiyd ya Ilaah? Kumfanyia Yeye Pekee ibada, dua, nadhiri na  Hukumu.

(فأعلم أنه لا إلاه إلا الله)

Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Allaah. (Muhammad: 19)

(فليكن أول ما تدعوهم اليه شهادة أن لا إله إلا الله)

Jambo la kwanza liwe mnapowalingania wao Kwake ni “Kuthibitisha kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allaah.

7- Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah? Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى.

 (ذلك بأن الله هو الحق وأن مايدعون من دونه الباطل )

Hivi ni kwa sababu hakika Allaah ndiye wa kweli, na hakika wanachokiomba ni cha uongo. (Luqmaan: 30)

(من قال لا إله إلا الله  وكفر بما يعبد من دون الله حرم ماله ودمه )

Atakayesema ‘Laa ilaaha illa Allaah  na akawapinga wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai(.

8- Nini maana ya Tawhiyd katika sifa za Allaah سبحانه وتعالى Kuthibitisha alivyojisifu Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى  au alivyosifiwa na Mtume wake.

 ) ليس كمثله شيء وهو السميعالبصير)

Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. (Ash-Shuwraa: 11) 

 (ينزل ربنا تبارك وتعالى في كل ليلة إلى السماء الدنيا)

Mola wetu Huteremka  kila usiku katika mbingu ya dunia.

9- Nini faida ya Tawhiyd kwa Muislamu? Kupata Hidaaya duniani na kuwa katika amani  Akhera.

 (الذين أمنوا ولم يلبسوا إيمانهم بظلم أولئك لهم الأمن وهم مهتدون )

Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma – hao ndio watakaopataamani na wao ndio walioongoka. (Al-An’aam: 82)

( حق العباد على الله أن لايعذب من لا يشرك به شيئ )

Haki ya mja kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى(Anayomfanyia) kuwaHamuadhibu yule asiyemshirikisha Yeye na chochote.

10- Je, Allaah سبحانه وتعالىyuko wapi? Allaah سبحانه وتعالى yuko mbinguni juu ya ‘Arsh.

 (الرحمن على العرش أستوى)

Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahma) Istawaa(Amelingamana sawa) juu ya ‘Arsh.(Tawahaa: 5)

إن الله كتب كتاباً إن رحمتي سبقت غضبي فهو مكتوب عنه فوق العرش )

Hakika AllaahAmeandika maandishi kwamba Rahma yangu imeshinda  ghadhabu  yangu, nayo yameandikwa  kumhusu Yeye juu ya ‘Arsh.

11- Je, Allaah سبحانه وتعالىyuko na sisi kwa dhati Yake au kwa elimu Yake? Allaah سبحانه وتعالى yuko na sisi kwa elimu Yake Anatuona na Anatusikia.

( قال لا تخافا إنني معكما أسمع وأرى)  

Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na Ninaona. (Twaahaa: 46).

(إنكم تدعون سميعا قريبا وهو معكم)

Hakika nyinyi mnamuomba Mwenye kusikia, Aliye karibu, na Yeye yuko pamoja nanyi.

12- Dhambi gani ni kubwa kabisa? Dhambi kubwa kabisa ni kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى

(يابني لاتشرك بالله إن الشرك لظلم عظيم)

Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa. (Luqmaan: 13)

(سئل أي الذنب أعظم؟قال أن تدعو لله ندا وهو خلقك )

Aliulizwa dhambi gani kubwa? Akasema ni kumuomba Allaah pamoja na mshirika Na hali Yeye ndiye Aliyekuumba.    

13- Shirki gani iliyokuwa kubwa? Kufanya ibada kwa kumuelekea asiye Allaahسبحانه وتعالى kama du’aa.

 )قل إنما أدعو ربي ولا أشرك به أحدا(

Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu, wala simshirikishi Yeye na yeyote. (Al-Jinn: 20)

(أكبر الكبائر الإشراك بالله)

Dhambi kubwa ni kumshirikisha Allaah.

14- Ni yapi madhara ya kumshirikisha Allaahسبحانه وتعالى? Kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى husababisha kudumu milele motoni.

(إنه من يشرك بالله فقد حرم الله عليه الجنة وماواه النار)

Kwani anayemshirikisha Allaah, hakika Allaah Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. (Al-Maaidah: 72)

(من مات يشرك بالله شيئا دخل النار)

Atakayekufa na huku amemshirikisha Allaahkwa chochote, ataingia motoni.

15- Je, Kitendo chema kinafaa kikiwa kimemshirikisha Allaahسبحانه وتعالى? Hakifai kitu kitendo ambacho kina kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى.

(ولو أشركوا لحبط عنهم ما كانوا يعلمون)

Na lau wangelimshirikisha yangeliwaharibikia waliyo kuwa wakiyatenda (Al-An’aam 88)

(من عمل عملا أشرك فيه معي غيري تركته وشركه)

Atakayefanya kitendo na huku kanishirikisha Mimi kwa kitendo hicho na mwengine, namwacha yeye na shirki yake.

16- Je, Shirki ipo kwa Waislamu? Ndio, ni masikitiko kuwa  ipo tena nyingi

(وما يؤمن أكثرهم بالله إلا وهم مشركون)

Na wengi katika wao hawamuamini Allaah pasina kuwa ni washirikina. (Yuwsuf: 106)

(لاتقوم الساعة حتى تلحق قبائل من أمتي بالمشركين وحتى تعبد الأوثان ) 

Qiyaamah hakitosimama mpaka kutafika wakati watu wa baadhi ya makabila katika ummah wangu wataungana na washirikina na hadi watakapoabudu asiye Allaah!

17- Nini hukumu ya kumuomba asiye Allaahسبحانه وتعالى kama Mawalii ‘Vipenzi vyake?  Kuwaomba ‘Mawalii’ ni shirki yenye kumpeleka mtu motoni.

(فلا تدع مع الله الها آخر فتكون من المعذبين) 

Basi usimwombe mungu mwengine pamoja na Allaah ukawa miongoni mwa watakaoadhibiwa.(As-Shu’araa  213)

(من مات وهو يدعو من دون الله ندا دخل النار)

Atakayekufa katika hali kumuomba asiye Allaahسبحانه وتعالى ataingia motoni.

18- Je, Kuomba du’aa ni ibada ya Allaah سبحانه وتعالى? Ndio, kuomba du’aa ni ibada ya Allaah سبحانه وتعالى.

(وقال ربكم أدعوني استجب لكم)

Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikien (Ghaafir 60)

(الدعاء هو العبادة )

Du’aa ni ibada.

19- Je, waliokufa wanasikia du’aa? Waliokufa hawasikii du’aa.

(إنك لا تسمع الموتى )

 (وما انت بمسمع من في القبور(

Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie.(An-Naml: 80)

Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini. (Faatwir: 22)

(إن لله ملائكة سياحين في الأرض يبلغوني عن أمتي السلام)

Hakika Allaah سبحانه وتعالىAnao Malaika wanaozunguka katika ardhi wakinifikishia salaam kutoka kwa ummah wangu.

20- Je, nafaa tuwaombe maiti na wasiokuwepo watuokoe? Hatuwaombi wao watuokoe bali tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى.

( اذ تستغيثون ربكم فاستجاب لكم)

Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu, naye Akakujibuni. (Al-A’araaf: 9)

(كان إذا أصابه هم أو غم قالياحي ياقيوم برحمتك أستغيث)

Alikuwa akifikwa na hamu au majonzi anasema ‘Ee uliye na uhai wa maisha, uliyesimamia kila jambo, kwa rahma Zako nakuomba uniokoe.

21- Je, Inafaa  kuomba msaada kwa asiyekuwa Allaah? Haifai kuomba msaada kwa mwengine asiye Allaah سبحانه وتعالى.

(إياك نعبد وإياك نستعين)

Wewe tu ndiye tunayekuabudu na Wewe tu ndiye tunayekuomba msaada. (Al-Faatihah: 5)

(إذا سألت فأسال الله وإذا أستعنت فأستعن بالله )

Unapoomba muombe Allaah na unapotaka msaada taka msaada kwa Allaah.

22- Je, Inafaa kuomba msaada kwa walio hai? Ndio kwa kadiri wanavyoweza.

(وتعاونوا عل البر والتقوى ولا تعاونوا على الإثم والعدوان)

Na msaidiane  katika wema na uchaji Allaah. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. (Al-Maaidah: 2)

(والله في عون العبد ما دام العبد في عون أخيه )

Allaah Yuko katika kumsaidia mja Wake maadam mja huyo yuko katika kumsaidia mwenzake.

23- Je, Inafaa  kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah سبحانه وتعالى? Haipasi kuweka nadhiri isipokuwa kwa sababu ya Allaah سبحانه وتعالى.

(رب إني نذرت لك ما في بطنيمحررا فتقبل مني )

Mola wangu! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. (Al-‘Imraan: 35)

 (من نذر أن يطيع الله فليطعه ومن نذر أين يعصيه فلا يعصه )

Anayeweka nadhiri kumtii Allaah basi amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah basi asimuasi.

24- Je, Inafaa  kuchinja bila kumkusudia Allaahسبحانه وتعالى? Haifai kuchinja kwa malengo yasiyo ya Allaah سبحانه وتعالى  kwa sababu ni shirki kubwa.

(فصل لربك وأنحر)

Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako. (Al-Kawthar: 2)

 (لعن الله من ذبح لغير الله 

Allaah Humlaani anayechinja kwa yasiyo makusudio kwa ajili ya Allaah.

25- Je, Inafaa kutufu makaburi? Haifai kuzunguka makaburi, bali kuzunguka (kutufu) Ka’abah pekee.

(وليطوفوا بالبيت العتيق )

Na waizunguke Nyumba ya Kale. (Al-Hajj: 29)

(من طاف بالبيت سبعا وصلى ركعتين كان كعتق رقبة )

Atakayezunguka Ka’abah mara saba kisha akaswali rakaa mbili ni kama mfano kamwacha huru mtumwa mmoja.

26- Je, Inafaa kuswali na kaburi liko mbele yako? Haifai kuswali kulielekea kaburi.

(فول وجهك شطر المسجد الحرام  (

Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu. (Al-Baqarah: 144)

(لاتجلسوا على القبور ولا تصلوا إليها)

Msikalie makaburi wala msiswali kuyaelekea.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s