Al-Khansaa Radhiya Allaahu ‘anha (Ummu Ash-Shuhadaa)

Jina  lake hasa ni Tamaadhwur Bint ‘Amru bin Ash-Shariyd bin Rabaah As-Sulaymiyyah. Alijulikana kwa jina la Al-Khansaa  na vile vile  Umm Ash-Shuhadaa (mama wa mashahidi) kutokana na watoto wake waliofariki katika jihaad. Pia alijulikana kuwa ni mwanamke mwenye haiba nzuri iliyojaa fadhila, tabia njema njema, ushujaa na subira kubwa.

 

Alipokuwa kabla ya kuingia katika Uislam, alikuwa akitunga mashairi ya beti mbili tatu hadi walipofariki kaka zake Mu’aawiyah na Swakhar bin ‘Amru, alifikwa na huzuni kubwa sana hata akawatungia mashairi. Yakawa maarufu, naye akawa mshairi maarufu kabisa. Inavyosemekana hakuweko mwanamke aliyekuwa hodari wa mashairi kama yeye.

 

Baada ya vifo vya kaka zake, alikuja kwa Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na watu wake wa Bani Sulaym akasilimu.

 

Ilipofika wakati wa vita vya Qaadisiyyah alidhihirisha subira yake kubwa alipokwenda vitani pamoja na watoto wake wanne wa kiume na akawausia kwa kuwaambia maneno haya mazito:

 

“Enyi watoto wangu, naapa kwa Yule Ambaye hakuna Apasaye kuabudiwa ila Yeye, nyinyi ni watoto wa baba mmoja, sikumkhini baba yenu, mmesilimu kwa kutii, mmehama kwa khiari yenu, …” hadi akasema “Mtakapoamka kesho Insha-Allah kwa salama, nendeni vitani kupigana na adui zenu, kwani mnajua Aliyowaandalia Allaah (Subhaana wa Ta’aala) ya thawabu nyingi kwa kupigana na makafiri. Tambueni kuwa nyumba ya milele (Pepo) ni bora kuliko nyumba ya kutoweka (Dunia), Anasema Allaah (Subhaana wa Ta’aala):

 

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اصْبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَاتَّقُواْ اللّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ))

  

 ((Enyi mlioamini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Allah, ili mpate kufanikiwa)) [Al-‘Imraan: 200].

 

Wakaenda vitani na alipopata habari ya vifo vyao wote alisema: “Alhamdulillah kwa Yule Aliyenipa heshima ya kuuliwa kwao na namuomba Allaah (Subhaana wa Ta’aala) Aniunganishe nao kwa Rahma Zake”.

 

Al-Khansaa (Radhiya Allahu ‘anhaa) alifariki katika Ukhalifa wa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allahu ‘anhu).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s