Swali: Kuoa Mke Wa Pili Bila Ya Mke Wa Kwanza Kujua?

Je inajuzu kwangu kuoa mke wa pili bila ya mke wa kwanza kujua kwa kuwa wa kwanza haridhii?

´Allaamah Swaalih as-Suhaymiy:

Kwa nini unasikia uoga? Kwa nini? Wengi wetu ni waoga katika masuala haya. [Wanasema] “Msiwaambie wanawake kwa kuwa hawatokubali hata Hadiyth.”

Ndugu wapenzi! Mke wa kwanza hana haki kukukataza au kukuingilia baina yako wewe na baina ya kuoa, lakini wewe sasa iulize nafsi yako. Ukikuta kwenye nafsi yako wewe ni mwanaume mwenye uwezo wa [kutekeleza] uadilifu na moyo wako ni wenye nguvu, na utaweza kuvumilia utayosikia na kukabiliana na maneno mengi, jitahidi kwanza kwa uadilifu, kisha ndio uoe zaidi. Ama ikikujia katika nafsi yako dhana kuwa utalemea moja kwa moja kwa [mke] mmoja na unakhofia matokeo mabaya, usifanye hivyo.

Mimi nafikiria ikifikia suala la wewe mpaka kukhofia utapomueleza hali itakuwa khatari sana – ni juu yako kuwa mpole kwake, panga utayomwambia, jitahidi kumuweka katika hali nzuri, mfurahishe kwa kitu chochote kama mali n.k. Kisha ukihakikisha ukaona kuwa hajaridhia, yaani haikuwezekana kukubaliana na wewe juu ya hilo, sio lazima kwake kukukubalia.

Na [wanaume] huisheni hii Sunnah! Wanawake wa Kiislamu wamekaa manyumbani, [mpaka] miaka ya kuolewa inapita. Baadhi ya manyumba yana wanawake kumi, miongoni mwao kuko wanaofika hadi miaka arubaini mpaka khamsini na wala hawajaolewa. Na sisi tumewaiga wamagharibi na tumekaa kazi tu ni kusikiliza filamu chafu – na mafilamu yote ni machafu ambayo yanashawishi suala la ndoa, ukewenza n.k. Na Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema

“… Basi oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane.” (04:3)

Kaanza kwa wake wawili. Na nnakumbuka kuwa Shaykh wetu Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na hata Salaf katika hili wanasema:

“Asili ni [kwa mwanaume kufanya] ukewenza.”

Kuondolewa ukewenza ni wakati wa khofu tu, khofu ya nini? Kutekeleza uadilifu tu. ALLAH ANAJUA ZAIDI.

WABILLAHI TOWFIIQ

Advertisements

2 responses to “Swali: Kuoa Mke Wa Pili Bila Ya Mke Wa Kwanza Kujua?

  1. Mashekhe hiz picha vipi tena, ina juzu?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s