JIHAAD IMEKUSANYA KILA AINA YA IBADA.

Jihaad imekusanya kila aina ya ibada za kiroho na kiwiliwili, kuikinai dunia, kuihama nchi na kuyahama matamanio na hii ndiyo maana ikapewa jina la ‘Uchaji Allaah’, kwani imekuja katika Hadiyth kuwa:

‘Ucha Mungu wa umma wangu ni Jihaad katika njia ya Allaah.”

Na ndani yake mna kuitakasa nafsi, kuitakasa mali, na kumuuzia Allaah nafsi, na haya yote ni matunda ya mapenzi na imani na yakini na kuelekea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).

Allaah Anasema:

إِنَّ اللّهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ مِنَ اللّهِ فَاسْتَبْشِرُواْ بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ وَذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Allaah – wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi Aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur-aan. Na nani atimizae ahadi kuliko Allaah? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.” At-Tawbah: 111

Dini ya Kiislamu imeitukuza ibada hii ya Jihaad, na ikatunabahisha juu umuhimu wake katika sura nyingi zilizoteremshwa Madina na ikawalaumu wanaoiacha na wanaoipinga na kuwapa sifa za unafiki na wenye maradhi moyoni.

ALLAH ANAJUA ZAIDI.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s