Vatican yakiri: Uislamu una wafuasi wengi zaidi duniani

Vatican yakiri: Uislamu una wafuasi wengi zaidi duniani
Vatican imetoa taarifa inayoashiria kasi ya kuongezeka idadi ya Waislamu katika mwaka mmoja uliopita na kukiri kwamba Uislamu una wafuasi wengi zaidi duniani kuliko Ukristo.
Serikali ya Vatican imesema katika taarifa hiyo kwamba Uislamu ndiyo dini iliyoenea zaidi duniani na imeupita Ukristo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa idadi ya Waislamu duniani imepita watu bilioni na kiwango hicho ni zaidi ya idadi ya Wakristo kote duniani.
Taarifa hiyo ya kituo kikuu cha kidini cha Wakatoliki imesema: “Vatican inakiri kwamba Uislamu ndio dini ya kwanza inayoenea kwa kasi zaidi katika maeneo mbalimbali duniani na asilimia 19 ya watu wote duniani ni Waislamu huku Wakristo wakiwa asilimia 17 na nusu.”
Taarifa hiyo ya Vatican pia imesema: “Licha ya propaganda zinazofanywa na wapinzai za kuchafua sura ya Uislamu na kiwango kikubwa cha fedha kinachotumiwa katika kuhubiri Ukristo kati ya Waislamu, lakini mvuto wa itikadi za Kiislamu kwa Wamagharibi wakiwemo Wakristo, Wayahudi na wafuasi wa dini nyinginezo katika miaka ya hivi karibuni, hauna kifani.”
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s