Jeshi la Osama bin Zeid

Baada ya kifo cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) , Abubakar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliona ni bora kulianzisha tena jeshi la Osama (Radhiya Allaahu ‘anhu), jeshi lililoundwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) mwenyewe chini ya uongozi wa Osama bin Zeid (Radhiya Allaahu ‘anhu), na jeshi hilo lilikuwa limekwishapiga kambi nje ya Madina likijitayarisha kwenda kupigana na Warumi, lakini kutokana na kushtadi kwa maradhi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) jeshi hilo halikuondoka.

Baada ya kifo cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) jeshi hilo lilirudi tena Madina, na Waislamu wakahitilafiana juu ya kulianzisha tena jeshi hilo.

Baadhi ya Waislamu akiwemo Omar bin Khatab (Radhiya Allaahu ‘anhu) waliona kuwa si fikra nzuri kulianzisha tena jeshi hilo hasa wakati huu ambapo mji wa Madina umo katika hatari ya kuvamiwa na makundi ya waliortadi.

Abubakar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema;

“Lianzisheni tena jeshi la Osama, kwani Wallahi hata kama mbwa wa mwitu wataninyakua basi nitalianzisha tena kama alivyofanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).”

Alipoona kuwa Abubakar (Radhiya Allaahu ‘anhu) ameshikilia jambo hilo, Omar bin Khattab (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema;

“Kwa vile Osama ni kijana mdogo sana, basi angalau ungemweka mtu mzima aliongoze jeshi hilo”.

Abubakar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliruka kutoka pale aliposimama na kuzishika ndevu za Omar bin Khatab (Radhiya Allaahu ‘anhu), akamwambia;

“Ole wako ewe Ibnil Khatab! Amepewa uongozi na Mtume wa Mwenyezi Mungu na wewe unanitaka mimi nimuondoe?”

Ndani ya jeshi hilo walikuwemo masahaba wakubwa kama vile Omar, Othman na wengine (Radhiya Allaahu ‘anhum), na lilipokuwa likiondoka mjini Madina, Abubakar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akawa analisindikiza huku akitembea kwa miguu na Osama (Radhiya Allaahu ‘anhu) akiwa amepanda farasi.

Osama (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye umri wake haukuzidi miaka kumi na nane wakati ule akasema;

“Ewe Khalifa wa Waislamu, bora wewe panda juu ya mnyama huyu na mimi nitakwenda kwa miguu”.

Abubakar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamjibu;

“Wallahi utabaki juu ya farasi na mimi nitatembea kwa miguu, kwani nitakuwa nimefanya jambo kubwa sana ikiwa nitaitia miguu yangu vumbi angalau kidogo katika njia ya Mwenyezi Mungu?.”

Kwa vile Abubakar alikuwa akiuhitajia ushauri na msaada wa Omar katika uendeshaji wa mambo ya Waislamu, na kwa vile Omar alikuwa miongoni mwa wanajeshi chini ya uongozi wa Osama, ilimbidi Abubakar amuombe Osama ili amruhusu Omar abaki naye Madina. Akamnong’oneza sikioni pake na kumwambia;

“Itakuwa vizuri kama utakubali kuniachia Omar, maana namhitajia katika kuendesha mambo ya Umma”.

Osama (Radhiya Allaahu ‘anhu), akakubali.

Abubakar (Radhiya Allaahu ‘anhu) angeweza kumuamrisha Osama (Radhiya Allaahu ‘anhu) juu ya jambo hilo, lakini hakufanya hivyo kwa sababu Osama (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa mkuu wa jeshi hilo na mwenye haki ya kutoa ruhusa hiyo, na kama Osama angelikataa, basi asingemlazimisha.

Na jambo hili la Abubakar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuliunda tena jeshi la Osama lilisaidia sana kuyavunja nguvu makundi ya walortadi na kuingiza uoga nyoyoni mwao, maana waasi hao walipoliona jeshi hilo likitoka nje ya Madina kuelekea Sham, walisema:

“Wallahi ungekuwa mji wa Madina uko katika udhaifu na hitilafu kama tunavyosikia, basi wasingeweza kulitoa nje jeshi kubwa kama hili kupambana na Warumi”.

Baada ya kuwasindikiza mpaka nje kidogo ya mji wa Madina, Abubakar akalihutubia jeshi hilo na kulijulisha juu ya misingi ya jeshi la Kiislamu linavyotakiwa liwe.

Baada ya kumshukuru na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, akasema:

“Msifanye khiyana wala msishambulie bila taarifa (ghadran), wala msikate kate maiti za adui, wala msiue mtoto wala mzee wala mwanamke, wala msiunguze mtende wala msikate mti unaotoa mazao wala msichinje mbuzi wala n’gome wala ngamia isipokuwa kwa ajili ya kula.

Na mtakutana na watu waliojitenga ndani ya hekalu zao kwa ajili ya ibada, basi waacheni hivyo hivyo walivyo.”

Kisha akasema: “Nendeni kwa jina la Mwenyezi Mungu.”

Haya ndiyo maamrisho ya Kiislamu, na hivi ndivyo alivyofundishwa Abubakar na Mwalimu wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Na hivi ndivyo majeshi ya kiislamu yalivyokuwa yakifanya kupitia karne zote.

Na waisome historia ya ufunguzi wa Kiislamu kama watakuta yale waliyofanya wao huko Algeria, Bosnia Kosovo, Afghanistan na hivi sasa Palestina. Waislamu wanachinjwa kama mbuzi na kukatwa katwa maiti zao na wengine wamezikwa wakiwa wazima, na wake zao wameingiliwa kwa nguvu na kuharibiwa, kisha wanajidai kuwa wao ni mabingwa wa kugombania haki za binadam

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s