Usihuzunike! Subira Katika Mitihani Ina Malipo Mema

Usihuzunike! Subira Katika Mitihani Ina Malipo Mema.

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

  ((وَالَّذِينَ صَبَرُواْ ابْتِغَاء وَجْهِ رَبِّهِمْ وَأَقَامُواْ الصَّلاَةَ وَأَنفَقُواْ مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلاَنِيَةً وَيَدْرَؤُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ أُوْلَئِكَ لَهُمْ عُقْبَى الدَّارِ)) ((جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَنْ صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَالمَلاَئِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ)) ((سَلاَمٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ))

 ((Na ambao husubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao na wakashika Swalah, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika Tulivyowapa; na wakayaondoa maovu kwa wema. Hao ndio watakaopata malipo ya Nyumba ya Akhera))  ((Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na waliowema miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango))  [Wakiwaambia] ((Assalaamu ‘Alaykum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyosubiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera)) [Ar-Ra’ad: 22-24]

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَعِينُواْ بِالصَّبْرِ وَالصَّلاَةِ إِنَّ اللّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ))

  ((Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na Swalah. Hakika Allah Yu pamoja na wanaosubiri)) [Al-Baqarah: 153]

 Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

 (( وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ))

  ((Na anayesubiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa)  [Ash-Shuuraa:  43]

Fadhila za subira zimetajwa sana katika Qur-aan na Hadiyth, na subira inahitajika katika kila vitendo vyetu, ikiwa ni vya ibada au vya nje ya ibada. Katika kuswali, kufunga, Hajj, kutoa mali kwa njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika maafa, maradhi, vifo vya watu wetu, katika kufanya da’awah, katika kuishi na wenzetu hasa inapokuwa kuna baadhi yetu tuna tabia nzito, katika kuishi katika mazingira tunapokuwa ugenini n.k.  

Muislam anapokumbwa na mitihani asihisi kuwa kaonewa, bali ni neema kwake kwani hivyo ni kuletewa adhabu duniani na kufutiwa dhambi kwa ajili ya mitihani hiyo ili kupunguziwa adhabu za Qiyaama. Vile vile ni dalili ya kupendwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kama zinavyosema Hadiyth zifuatazo:

 

Anapendelewa kheri na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)

وعن أنس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((إذا أراد الله بعبده الخير عجل له العقوبة في الدنيا وإذا أراد الله بعبده الشر أمسك عنه بذنبه حتى يوافي به يوم القيامة)) الترمذي

 Kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Anapompendelea kheri mja Wake, Humharakishia adhabu duniani. Na Anapomtakia shari mja Wake, Huzuia dhambi zake ili Amlipe siku Ya Qiyaama)) [At-Tirmidhiy]

 Hadiyth zifuatazo zinatuthibitishia kuwa mja anapopatwa na msiba hufutiwa madhambi yake:

 وعن أبي هريرة  رضى الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((ما يزال البلاء بالمؤمن والمؤمنة في نفسه وولده وماله حتى يلقى الله تعالى وما عليه خطيئة))  رواه الترمذي

 Abu Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu) amesema: ((Muumini mwanamume na Muumini mwanamke huendelea kupata mitihani katika nafsi yake, na mtoto wake na mali yake hata anakutana na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) akiwa hana dhambi)) [At-Tirmidhiy)

عن أبي سعيد و أبي هريرة رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((ما يصيب المسلم من نصب ولا وصب ولا هم ولا حزن ولا أذى ولا غم حتى الشوكة يشاكها إلا كفَّر الله بها من خطاياه )) رواه البخاري و مسلم

 Abu Sa’iyd na Abu Huraryah (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) wamepokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amesema: ((Muislam hatopatwa na tabu, wala maradhi wala hamu wala huzuni wala udhia wala ghamu (sononeko) mpaka mwiba unaomdunga isipokuwa Allaah Humfutia dhambi zake kwa sababu ya hayo)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Ni dalili pia ya mapenzi ya Allah kwa mja Wake:

 

 

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال  رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((مَنْ يُرِدْ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا يُصِبْ مِنْهُ)  صحيح

البخارى

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anayependelewa na Allaah (basi Allaah) Humpa msiba)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 و قال النبي صلى الله عليه وسلم: (( إن عظم الجزاء مع عظم البلاء، وإن الله تعالى  إذا أحب قوما إبتلاهم، فمن رضي فله الرضا ، ومن سخط فله السخط))     رواه الترمذي

   Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Malipo makubwa yako pamoja na balaa kubwa. Hakika Allaah Anapowapenda watu, Huwapa mitihani. Atakayeridhika basi atapata Radhi (Za Allah) na atakayechukia atapata Ghadhabu)) [(At-Tirimidhy]

 Faida za kukumbwa na mitihani:

·         Kufutiwa dhambi na maovu,

·         Kupandishwa daraja kwa kuzidishiwa imani yake mja kwa kuridhika kwake na mitihani,

·         Sababu ya kumfungulia mja milango ya kuomba tawbah kwa kumkumbuka Mola wake Aliyempa mitihani,

 

 ·         Kuimarisha mawasiliano na Allaah na kujikurubisha zaidi kwa Allaah kwa kumkumbuka na kumuomba Amuondelee mitihani hiyo na  Amlipe mema,

·         Kuzidi imani mja kwa kuamini yanayatokea ni Qadhwaa na Qadar ya Mola wake na sio kulalamika na kukufuru bali kushukuru na kuamini kuwa hakuna mwenye kuweza kumnufaisha au kumdhuru isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)

·         Kuwafikiria walio chini yake wenye mitihani mikubwa zaidi.

Yote hayo na zaidi ya hayo ni mafunzo ya mitihani katika kusubiri kwani hivyo ndivyo Anavyotaka Mola wetu kutujaribu Atuone nani katika sisi atakayeweza kusubiri Amlipe kheri zake, nani mkweli nani mnafiki, na nani mwenye imani ya kuamini Qadhwaa na Qadar ya Mola Wake:

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

 

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ  ((الم ))  ((أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ))   ((وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ))  

 

Kwa Jina la Allaah, Mwingi Wa Rehma, Mwenye Kurehemu daima

 ((Alif Laam Miym)) ((Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe?))   ((Hakika Tuliwajaribu waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Allaah Atawatambulisha walio wa kweli na Atawatambulisha walio waongo)) [Al-‘Ankabuut: 1-3]

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atuwezeshe kuwa na subira katika kila mitihani Yake ili Atulipe hayo yote tuliyoahidiwa katika kauli Zake na za Mjumbe Wake Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s