Kuhusu RIBA

Akipewa Riba Benki Achukue Kisha Awape Maskini Au Aache

SWALI:

Assalaam alaykum

Bismilah Rahman Rahim

Kwanza nakutakieni kila la kheir katika kulitayarisha na kuliborosha jarida letu, Amin Suala langu nauliza juu ya uwekaji/kuhifadhi pesa bank ambazo zina mfumo wa riba jee inafaa katika sheria zetu za kiislaam? Nina maana kwa mfano;

1-kama nitakatwa riba au

2-kupewa riba sitaichukuwa au

3-kama nitaichukua basi nitawagaia maskini Naomna unifahamishe ktk mitazamo yote Shukran.

wasalaam alaykum.

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kupewa riba ya kutoka benki.

Riba imekatazwa kwa njia kali na Uislamu, kwani Qur-aan inatufahamisha kuwa mwenye kula riba amejiandalia vita dhidi ya Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Kwa hiyo, haifai kuchukua riba unapokopesha wala kutoa unapokopeshwa. Na kawaida katika benki hizi za kawaida watu hawakatwi riba, riba inakatwa tu ikiwa umekopesha kutoka kwa benki. Kwa minajili hiyo, Muislamu hafai kuchukua mikopo yoyote ambayo ina riba ndani yake pindi utakapoilipa. Mara nyingi ukiweka akaunti yako kila baada ya mwaka au nusu, huongozewa riba katika akaunti yako kwa kiwango maalumu wanachojua benki na kuwaambia wateja wao. Hii pesa ya ziada unayowekewa ni haramu kwako kuitumia. Baadhi ya Wanachuoni wanaona kuiacha pia haifai kwani benki nyingi ni za wasiokuwa Waislamu, na riba hiyo husaidia katika kuupiga vita Uislamu ulimwenguni. Kwa msingi wa Kifiqh: Akhaffudhw Dhwararayn (Dhara lililo dogo), inafaa kwako uichukue kisha uitumie kwa faida ya labda kujenga choo, mitaro, barabara, na mengineyokama hayo, lakini zisiwe ni zenye kukunufaisha wewe kwa chochote. Pia usitarajie thawabu, Allaah Aliyetukuka ndiye Mwenye kujua hali yako hiyo.

Na Allaah Anajua zaidi.

Ujumbe wa ‘Iisa (‘Alayhis Salaam).

Riba

Kwa kushika na kuthibitisha sheria, Nabii ‘Iisa (‘Alayhis Salaam) alipinga kutoa au kuchukua riba kwa sababu matini ya Taurati kwa uwazi kabisa inakataza riba. Imenukuliwa katika Kumbukumbu la Sheria 23: 19 kuwa, “Usimkopehe ndugu yako Muisraeli kitu kwa riba; usimtoze riba juu ya mkopo wa fedha, chakula au chochote ambacho watu hukopesha kwa riba

Riba pia imekatazwa vikali sana katika Suratul Baqarah (2): 278 ya Qur’ani:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اتَّقُواْ اللّهَ وَذَرُواْ مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Enyi Mlioamini! Mcheni Allah, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini”.[Al-Baqarahh 278]

Ili kutekeleza sharti hili la Mwenyezi Mungu, Waislamu wameanzisha mfumo mbadala wa banki, inayojulikana kwa kawaida ‘Banki ya Kiislamu’, ambayo haina riba.

Hata hivyo, ayah inayofuata hii, Mayahudi walitoa ruhusa kukopesha kwa riba kwa wasiokuwa Wayahudi: “Unaweza kutoza riba unapomkopesha mgeni, lakini ndugu yako Muisraeli usimtoze riba, naye Mwenyezi Mungu, Mungu wako atakubariki katika shughuli zako zote utakazofanya katika nchi ambayo unakwenda kumiliki” (Kumbukumbu la Sheria 23: 20).

Kuchukua Mkopo Katika Benki Za Riba Ikiwa Hakuna Benki Za Kiislamu Inafaa?

SWALI LA KWANZA:

MIMI NAISHI SKANDINAVIA NINA SWALI. KUHUSU RIBA NI HIVI HUKU SKANDINAVI BENKI ZA HUKU HUKOPA WATU PESA KAMA 3000 ALAFU WANATAKA URUDISHE 3300 SASA. HII PIA UKIKOPA NI RIBA HATA KAMA UNAMATATIZO. HUNA ELA HAKUNA MTU WA KUKUKOPA. UKIKOPA HAPO BENKI NI HARAM.

SWALI LA PILI:

Asalam aleykum mi nauliza kamanimekopa gari bank na nalipa pamoja na riba je inafaa kwa mwislam kukopa bank? Je na kama hakuna taasisi ya kukopa bila riba tufanyeje naomba msaada kwa hilo

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuchukua mkopo wa riba. Mkopo wowote unaokopa na kulipa juu yake ziada ni riba kisheria na haifai kwa Muislamu kuchukua mkopo aina hiyo. Nchi za Scandinavia zinajulikana kuwa na Waislamu wengi kwa wakati huu wa sasa. Unalohitajia kufanya kwa sasa ni kujaribu kutafuta markaz (centre) na uwe na ndugu zako kwa hali na mali katika kufanya mambo ya Kiislamu.

Hata hivyo, sheria ya Kiislamu inamuangalia kila mmoja na tatizo alilo nalo. Ikiwa hali yenyewe ya hilotatizo ni mas-ala ya uhai na kifo basi unaruhusiwa kuchukua mkopo wa riba kutoka kwa benki baada ya kufanya juhudi ya kutafuta mkopo usiokuwa na riba. Ikiwa juhudi zako zimeruka patupu hapo utaruhusiwa kwa ajili ya kuokoa maisha na huku unachukukiasana. Suala hilo ni kama mfano wako kuwa katika sehemu ambayo hakuna chakula kabisa nawe uko katika hali ya kushurutishwa kula nguruwe kwani hakuna chakula kingine isipokuwa nguruwe. Wakati huo utakula nguruwe kwa kiasi cha kuokoa maisha yako.

Lakini haya matatizo tuliyo nayokama kutaka kununua nyumba, gari au vitu vingine ambazo kuzikosa hazitakupelekea wewe kuwa katika hali ya kukaribia kifo Uislamu umekataa kabisa mkopo wa aina hiyo.

Wengi wanaochukua mkopo wa benki si wenye kuwa na shida ya uhai na kifo, huchukua kwa mahitaji yao ya ziada ya kilimwengu kama tulivyoona hapo kuhusu kuchukua gari kwa mkopo na kulipa riba, au kuchukua nyumba za za mkopo kwa kulipa kidogo kidogo kwa miaka mingi ambazo ni mogeji (mortgage) na mahitaji mengineyo ya zaida ya kidunia.

Kwa hiyo, mikopo yoyote ya aina hiyo haifai kabisa kisheria. Na tumuogopesana Allaah kwa kuingia kwenye ribaa ambayo madhambi yake ni makubwa na adhabu zake ni kali mno.

Hakika ni kuwa Allaah Aliyetukuka Ametangaza vita na yeyote anayechukua riba pale Aliposema:

Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Allaah na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe” (Al-Baqarah: 278-279).

Na Allaah Anajua zaidi


3 responses to “Kuhusu RIBA

  1. Mbona nafuta video za mashekh wengne sizipati, mafano SHEIKH ROGO,SHEKH SAMIIR KHAN, SHEIKH MUSSA KILEO,SHEKH NURU MAULANA NA MASHEKH WENGNE WA MASHARIKI YA KATI,ASIA NA ULAYA.

  2. Mbona natafuta video za mashekh wengne sizipati, mafano SHEIKH ROGO,SHEKH SAMIIR KHAN, SHEIKH MUSSA KILEO,SHEKH NURU MAULANA NA MASHEKH WENGNE WA MASHARIKI YA KATI,ASIA NA ULAYA.

  3. ABDILLAH SALMIN MLAPAKOLO

    assalam aleykum swali langu kuna tofauti gani ktk kufanya biashara kama unanunua kitu alfmoja alafu una uza elfu mbili au tatu hii biashara au riba na mtu anayekopa tigo mathalani anakop 500 analipa 550 hii inaruhusiwa je na biashara iliyoruhusiwa ikoje?

Leave a reply to ABDILLAH SALMIN MLAPAKOLO Cancel reply