Uuzaji Wa Pesa (Swarf) na Kutuma Pesa Ni Halal?

Uuzaji Wa Pesa (Swarf) na Kutuma Pesa Ni Halal?
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Suala la Bureau de change

Uuzaji wa pesa (fedha) katika fiqihi waitwa swarf

Hii biashara ya ubadilishaji wa pesa toka kwa pesa (‘umlah) za nchi moja kwa pesa au za nchi nyengine yajuzu kwa msingi wa haja.

Allaah Ameihalalisha biashara hii kwa kuwa binadamu wanahitajia kubadilishana sarafu.

Swarf yajuzu kwa mujibu wa Hadiyth iliyopokelewa na ‘Umar bin Al-khatwaab na Abu Sa’iyd al-Khudry, na ‘Ubaadah bin Swaamit (Riwaya tofauti tofauti) [Radhiya Allaahu ‘anhum] “Msiuze dhahabu kwa dhahabu isipokuwa kiasi kile kile, wala fedha kwa fedha ila kiasi kile kile, na uzeni dhahabu kwa fedha au fedha kwa dhahabu mpendavyo” al-Bukhaariy na Muslim

Pesa (‘umlah) zinashirikiana na fedha na dhahabu na mali nyengineyo kwa kuwa ni thamani na kuna aina nyengine ambayo ya mali ambayo ni Muthman (kinacho nunuliwa).

Mali ambayo ni aina ya thamani: yabadilishwa kwa shuruti zifuatazo:

a- Ikiwa ni aina moja ya mali mfano dhahabu kwa dhahabu lazima iwe kiwango/gramu sawa baina zote mbili;

b- Ikiwa ni mali tofauti hakuna neno ikiwa kuna tofauti baina kiwango mfano dhahabu gramu tano kwa fedha gramu kumi.

c- Ikiwa ni aina moja lazima sarfu iwe papo hapo. Mfano, Ikiwa utapokea dola malipo yake lazima yawe papo hapo, na haikubaliki kuchelewesha japo kwa lisaa.

Ama mas-ala ya kutuma pesa toka nchi mmoja hadi nyengine mji kwa mji haina neno kwa sababu aliyetuma ananunua/kulipia huduma za kutuma fedha zake nchi moja hadi nyengine. Na hapa hayaingii mas-ala ya riba.

Wakati mtu anakwenda kutuma pesa kwa za nchi za nje hufanya swarf kwa shillingi za Tanzania au nchi nyingine. Hii inachukuliwa kuwa amefanya swarf na qabdh (kuzimiliki) fedha kumepatikana.

Kisha sasa analipia khidmah (huduma) za kutuma pesa na hili si jambo la ingia ndani yake riba. Ni mfano wa mtu aje kwako akupe paundi mia akwambie wewe waenda likizo bara Afrika nifikishie kwa mke wangu mfano kisha akulipishe kwa huduma hii haya ni mas-ala ya ijara na si ya uuzaji.

Na kwa msingi huu hakuna suala la kupokea zile fedha siku ile au wakati ule ule.

Wa Allaahu A’alam

By Ahmed

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s